🔺️AHAIDI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU KWA WANAFUNZI ILI KUPATA ELIMU STAHIKI KATIKA MAZINGIRA RAFIKI.
"Matumizi ya fedha za mfuko wa Jimbo katika kuchangia Elimu ili kukuza, kuimarisha na kuendeleza elimu, leo nimegawa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 66 kwa shule za msingi na sekondari wilayani Butiama, ikiwa ni hatua ya kuboresha mazingira ya kufundishia kwa walimu na kujifunzia kwa wanafunzi wetu". Ameeleza Dkt. Mahera.
"Katika zoezi hilo, tumekabidhi bati, misumari, saruji na mbao kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya elimu katika jimbo letu. Aidha, tumetoa vitabu vya masomo ya Sanaa na Sayansi kwa Shule za Sekondari vyenye thamani ya shilingi 2,700,000/= ili kuongeza ubora wa ujifunzaji na kuinua ufaulu wa wanafunzi". Ameongeza Dkt Mahera.
“Tutaendelea kushirikiana na kuhakikisha watoto wetu wanapata elimu bora katika mazingira rafiki na yenye motisha”. Amesisitiza Dkt. Mahera.








Comments
Post a Comment