DKT. MWIGULU AAGIZA KUJENGWA KWA LAMI BARABARA YA KM 1.5 ILI KUFIKA HOSPTALI YA WILAYA YA ARUSHA AWAPA JUKUMU TARURA.
🔺️AKERWA NA VIONGOZI KUSHINDWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI KWA WAKATI.
🔺️APIGA MARUKU UPUNGUFU WA VYOO MASHULENI NA KWENYE ZAHANATI.
🔺️AAGIZA KUSHUGHULIKIWA KWA WAKANDARASI WANAO NYANYASA WAFANYAKAZI NA KUTOWALIPA.
Dkt. Mwigulu ameeleza kuwa siyo jambo jema kuona wanawake wanao kwenda kujifungua hosptalini hapo kuteseka na barabara yenye urefu mdogo kufika hosptalini hapo kitu ambachi kinaweza kuleta athari kubwa pindi mama mjamzito anapopita kwenye makorongo na barabara korofi ambacho ni kipande kidogo kufika hosptali hiyo ya wilaya.
"Siyo jambo jema kunao mama zetu wanapokwenda kujingua kuteseka na barabara kipande kidogo hicho ambacho hakina lami wakati Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan amejenga Hosptali ya kisasa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora". Amesema Dkt. Mwigulu.
"Nakuagiza Meneja Tarura Mkoa wa Arusha kuanza mchakato wa kutangaza tenda ili kumtafuta mkandarasi atakaye jenga kipande hicho haraka iwezekananvyo ili kuweza kuondoa adha hiyo kwa wananchi, Pia waziri wa Ujenzi hakikisha fedha zinapatikana kwa wakati ili kuweza kukamilisha mchakato huo". Amesisitiza Dkt. Mwigulu.
![]() |
| Pichani hii ni moja kati ya shule 21 za Wasichana zilizojengwa nchi nzima na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan. |
Akizungumzia sekta ya elimu, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ametoa maagizo kwa halmashauri zote nchini kuanzia bajeti mpya hataki kusikia upungufu wa matundu ya vyoo katika shule zote za serikali nchini pamoja na zahanati zote."Zaidi ya Wilaya 100 zilikuwa hazna hosptali za Wilaya lakini katika Kipindi cha miaka 4 ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameweza kujenga hosptali 169, Zahanati 2700, Pamoja na hayo pia alikuta mashine vya MRI katika nchii zipo 16 tu lakini ameweza kununua zingingi 32 kitu ambacho kinafanya kila hosptali ya mkoa na zile za kanda kuwa na MRI pamoja na vifaa tiba vingine vya kisasa". Amesema Dkt. Mwigulu.
"Katika Sekta ya elimu Rais Dkt. Samia ameweza kujenga maalumu za wasichana kila mkoa, shulee za amali 103, shule za kawaida 1300 kitu ambacho kina sogeza elimu karibu na jamii lakin siyo kujenga tu ni pamoja na kuweka watumishi ambao watawahudumia wanafnzi hao ndiyo maana ametoa ajira za walimu wapya zaidi ya elfu 12". Ameongeza Mwigulu.
Akizungumzia swala la utatuzi wa changamoto za wananchi Dkt. Mwigulu ameleza kuwa anachukizwa na jinsi baadhi ya vingozi wanavyo shindwa kutatua changamoto za wananchi na kupelekea kupoteza haki zao za msingi."Sitaki mazoeaa katika utatuzi wa kero za wananchi, Hatukupelekwa maeneo mengi ya utawala ili kugawana vyeo, nataka kila mmoja ajishikilie kwenye majukumu yake sitakuwa na mbao ya kuvumiliana hawa wananchi wanateseka na nyie mpo mmepewa na fasi za kuwahudumia wananchi nasiyo vinginevyo". Amesisitiza Dkt. Mwingulu.
Aidha pia Dkt. Mwigulu ameupongeza Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. Mwinyi A. Mwinyi kwa usimamizo wa miradi pamoja na uongozi mzima wa Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana kwa pamoja na kulidhishwq na ripoti ya miradi yote ya Wilaya ya Arusha.
Pia ameomueleza Dkt. Mwigulu jimbo hilo limekuwa na uhaba wa barabara unganishi kuwa mbovu licha ya barabara zingine kuunganishwa hadi kwenye vivutio mbalimbali vya utalii kitu ambacho kinakosesha halmashauri hiyo mapato na kunyima fursa kwa wananchi ya ufanyaji wa biashara.











Comments
Post a Comment