SASA NI MARUFUKU USAFIRIASHAJI HARAMU KWENYE VITUO VYA MABASI SERIKALI YAWEKA MADAWATI TA USTAWI WA JAMII KUDHIBITI.
KATIKA kupambama na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto serikali imeanzisha madawati 115 ya kupinga ukatili katika masoko mbalimbali kwenye mikoa 12 na halmashauri 88 nchini na kuimarisha ulinzi katika vituo vya mabasi kwa lengo la kuwasaidia waathirika na kuazuia usafirishaji haramu na vitendo vya ukatili.
Dkt. Theresia alisema pia serikali imefanikiwa kuweka mabango 8,015 yanayopinga ukatili katika maeneo mbalimbali ya serikali za mitaa, pamoja na kufanya midahalo 4,748 kuhusu sababu za ukatili na mbinu za kuzuia ukatili.
Aidha ameeleza kuwa wamefanikisha kufanyika kwa mikutano 61,387 ya kujadili masuala ya ukatili,katika vijiji 29 kati ya vijiji 12319 sawa na asilimia 0.24 ambapo ambavyo vimetunga sheria ndogo za kupinga vitendo vya ukatili.
"Tumeanzisha madawati ya Ustawi wa Jamii katika vituo vya mabasi kwa lengo la kuasaidia waathirika na kuwazuia usafirishaji haramu na vitendo vya ukatili".Amesema Dkt. Theresia.
Licha ya kuzungumzia mafanikio hayo,alisema bado serikali ina kazi kubwa ya kufanya hususan katika kuongeza kasi ya utungaji wa sheria ndogo katika vijiji vyote na kuimarisha uratibu na ufuatiliaji wa utekelezaji.
"Mbali ya mpango kazi wa kitaifa wa kutokomeza ukatili wa kijinsia pia tumekuwa tukihamasisha usawa wa kijinsia kwa lengo la kuzikomboa jambii kuachama na upotovu wa utandawazi wa dunia hii kwa lengo kutoa haki kwa pande zote". Amesema Lucy.
"Pia Ushiriki wetu katika kikao kazi hiki, ni kusapoti mipango ya serikali ya Tanzania ili kuhakikisha utekelezaji wa mpango kazi wa Kitaifa unakwenda vizuri hasa tukijikita zaidi kwenye suala la mazingira salama katika maeneo ya jumuiya". Ameongeza Lucy.
Aidha ameeleza kuwa kwa mujibu wa takwimu za kidunia na za kitaifa tatizo la ukatili wa kijinsia bado liko, hivyo imesababisha serikali kuweka nguvu katika mapambano na udhibiti wa vitendo vya ukatili ikiwamo kutunga sera na sheria nzuri za kuzuia matukio hayo.




Comments
Post a Comment