đź’˘MWONGOZO UTAKAO WASAIDIA WANAHABARI NA WATENGENEZA MAUDHUI KUJUA MAADILI NA MIIKO YA JAMII ZA PEMBEZONI.
Juma alisema katika katika siku za karibuni wameibuka watengeneza maudhui wa ndani nan je ya nchi, Kwenda moja kwa moja katika maeneo ya jamii hizo hasa Wahadzabe na kutoa maudhui yao bila ridhaa yao na maudhui mengine ambayo ni kinyume cha maadili.
“Kutokana na changamoto hii, MAIPAC kwa kushirikiana na UNESCO na Idara ya Habari Maelezo wanaandaa mwongozo maalum wa kufanyakazi katika jamii hizi kwa kuzingatia maadili na bila kudhalilisha utu wa jamii hizi”alisema
Alisema sambamba na mradi huo, pia MAIPAC kwa kushirikiana na UNESCO ,Maelezo na SAVVY Media, wanatarajia kusaidia jamii hizi kujua matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii lakini pia kuanza kunufaika na matangazo na Habari ambazo zimekuwa zikitangazwa.
“Tutazijengea uwezo jamii hizi, kuweza kutumia vizuri mitandao kwa manufaa yao pia kiuchumi na kutambua haki zao mbali mbali za kidigitali na hivyo kuinua Uchumi wao”alisema
Wakizungumza katika mjadala huo, baadhi ya watengeneza Maudhui mitandaoni na Maafisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA),walisema matumizi ya mitandao na akili unde vinapaswa kusaidia vijana na jamii badala ya kuopogwa.
Samboga alisema jamii yao imepata umaarufu mkubwa katika mitandao ya kijamii katika siku za karibuni lakini hata hivyo hainufaiki na wanaotengeneza picha na Habari.
“Wanakuja wanatupiga picha na kutuhoji tunasikia mijini tunaonekana sana lakini sisi hatunufaiki zaidi ya kupewa pombe, sasa tunaomba kusaidiwa kunufaika”alisema





Comments
Post a Comment