💢SASA KABUMBU KIPIGWA ARUSHA KUTOKA MATAIFA YA AFRIKA, NYASI ZIATASEMA KWELI.
Kasi ya maandalizi ya miundombinu ya michuano ya Africa Cup of Nations 2027 imeingia katika hatua mpya baada ya Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba, kutoa agizo kali kwa mkandarasi kuhakikisha ujenzi wa barabara za kuelekea uwanja wa AFCON jijini Arusha unafanyika mchana na usiku bila kusimama.
Ziara hiyo ya kushtukiza iliyofanyika Aprili 17, 2026 imelenga kukagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja pamoja na miundombinu yake, huku presha ikiongezeka kutokana na ujio wa wakaguzi kutoka Confederation of African Football wanaotarajiwa kuwasili hivi karibuni.
Ingawa baadhi ya maeneo yanaonesha mafanikio, Waziri Mkuu hakusita kueleza wazi kuwa kasi ya ujenzi wa barabara bado iko chini ya kiwango kinachohitajika.
WAZIRI MKUU AMTAKA MKANDARASI ANAYEJENGA BARABARA ZA KUELEKEA UWANJA WA AFCON KUONGEZA KASI.
Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba amemuagiza Mkandarasi anayejenga barabara zinazoelekea kwenye Uwanja wa mpira wa miguu Arusha, maarufu uwanja wa AFCON kufanya kazi usiku na mchana ili ujenzi huo uweze kukamilika kwa wakati kwa kuzingatia wakaguzi wa Uwanja huo watakuja kabla ya mashindano hayo kufanyika mwaka 2027.
Dkt Mwilugu ametoa rai hiyo leo Aprili 17,2026 wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo, licha ya kuridhishwa na utekelezaji wa mradi huo, amemuagiziza Mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara ili zikamilike kabla ya mwezi Mei mwaka huu 2026.
Aidha, amesisitiza ujenzi huo wa barabaraba uzingatie vigezo na viwango vinavyozingatia matakwa ya mradi huo wa uwanja, ili wakaguzi kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) hawapati dosari yoyote watakapofika kwa ajili ya ukaguzi.
Aidha meweka wazi kuwa ujenzi wa barabara hizo pia uzingatie viwango vinavyotakiwa ili kuhakikisha zinakidhi mahitaji ya wananchi wanaoingia na kutoa uwanjani sambamba na wananchi kupa thamani halisi ya fedha zao na pia kuepusha hoja za wakaguzi wa CAF.
"Ninawaagiza kufunga kamera kwa wingi katika maeneo yote ya uwanja huo pamoja na viwanja vingine vya michezo ambavyo vitatumika ili kudhibiti vitendo visivyofaa ikiwemo imani za kishirikina katika michezo". Amesisitiza Dkt.Mwigulu
Hata hivyo, ameonya tabia ya baadhi ya wakandarasi kuchelewesha kazi na wengine kutolipa wafanyakazi na vibarua wanaofanya kazi kwenye site zao, na kusisitiza kuwa haitavumilia tabia hizo na yeyote atakayekiuka maelekezo hayo atazuiwa kushiriki katika miradi mingine ya Serikali.
Awali, Dk, Waziri Mkuu hakusita kumpongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake na mapenzi yake ya dhati ya kuleta mageuzi ya maendeleo nchini, huku akibainisha kuwa Dkt. Samia ameandika historia kwa kuandaa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya miaka 25 ijayo pamoja na kufanya maboresho makubwa katika mitaala ya elimu-jambo lililowahi kufanyika mwaka 1967 wakati wa uongozi wa Julius Kambarage Nyerere.







Comments
Post a Comment