KIHONGOSI KUTUA ARUSHA, CCM YAWEKA WAZI JUU YA UJIO WAKE.

đź’˘ATAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA WILAYA 3.

Na Lucas Myovela - Arusha.

Chama cha mapinduzi Mkoa wa Arusha imewwka wazi juu ya ujio wa katibu wa siasa,mafunzo na uenezi wa chama hicho taifa Ndg. Kenani Kihongosi ambapo anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi na kukagua miradi ya maendeleo kwa wananchi inayotekelezwa na serikali ya awamu 6 chini ya Rais Dkt. Samia Sulluhu Hassan.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa CCM Mkoa wa Arusha, Saipulan Ramsey, ametangaza rasmi ujio wa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenan Kihongosi, ambaye anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi mkoani humo kuanzia tarehe 4 mwezi huu.


Ramsey amesema kuwa ziara hiyo itakuwa ya siku 3 na itaanzia Wilaya ya Karatu siku ya tarehe 4, na siku tarehe 5 ni Arumeru na kisha kumalizika katika wilaya ya Arusha Jiji siku ta tarehe 6/6/2026.


Ameeleza kuwa lengo la ziara hiyo ni kufanya mikutano kwenye mashina ya CCM kwa ajili ya kukagua uhai wa chama, kuimarisha shughuli za kisiasa na kusikiliza maoni ya wanachama. Aidha, Kihongosi atatembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Chama Cha Mapinduzi pamoja na Serikali.


Vilevile, ziara hiyo inalenga kusikiliza, kufuatilia na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi katika maeneo atakayoyatembelea, sambamba na kuhimiza ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo.

Kwa mujibu wa Ramsey, Katibu huyo wa Taifa atafanya mikutano ya hadhara katika kila eneo atakalofika ili kutoa fursa kwa wananchi kueleza changamoto zao moja kwa moja na kupata ufafanuzi pamoja na majibu ya masuala yanayowagusa.


Aidha Chama cha mapinduzi Mkoa wa Arusha kimewahimiza wanachama na wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mikutano hiyo ili kuwasilisha maoni, changamoto na mapendekezo yao kwa viongozi wa chama na serikali.

Comments