π’MBUNGE MARRITA AMSHUKURU RAIS DKT. SAMIA KUENDELEA KUWEKEZA NAKUMALISHA MIRADI YA WANANCHI.
π’KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE AKOSHWA NA MIRADI KUENDANA NA THAMNI YA FEDHA.
Na Lucas Myovela - Arusha.
Menge wa wa Uhuru umetua Jiji la Arusha leo Julai 9, 2026 ikiwa ni muendelezo wa kukikimbizwa katika ufunguzi,uwekaji wa mawe ya msingi pamoja na ukaguzi mbalimbali wa miradi ya serikali na binafsi katika Mkoa wa Arusha katika wilaya zote 7 za Mkoa huo.
Mwenge wa uhuru ukikagua miradi saba katikati Jiji la Arusha yenye thamani ya shilingi Bilioni 3.9 chini ya kiongozi wa mwenge kitaifa kwa mwaka 2026 Ndg. Wazo Mwang'onda.
UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI KATIKA MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA GIRIKI - SAKINA ILI KUONDOA KERO YA MAFURIKO KWA WANANCHI.
"Ujenzi wa Barabara ya Giriki katika Kata ya Sakina unatarajia kuondoa kwa changamoto ya mafuriko ambayo imekuwa ikiwasumbua wananchi kwa muda mrefu, hasa wakati wa mvua kubwa". Amesema Mwang'onda.
Akizindua jiwe la Msingi Kiongozi wa Mbio za Uhuru Kitaifa mwaka 2026,Wazo Mwang'onda wakati wa kukagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Giriki yenye urefu wa kilomita 1.1 kiwango cha zege katika Jiji la Arusha ili kuondoa kero za wananchi ambapo wqnapatwa na mafuriko katika kipindi cha msimu wa mvua.
Mwang'onda ameeleza kuwa ujenzi huo unalenga kuboresha miundombinu ya barabara na mifereji ya kupitisha maji, hivyo kurahisisha usafiri, kulinda makazi na mali za wananchi pamoja na kuboresha mazingira ya shughuli za kijamii na kiuchumi.
"Tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha anatatua changamoto ya barabara hii ambayo awali wananchi walikuwa wakisumbuliwa na mafuriko". Amesema Mwang'onda.
Kwa upande wake Meneja wa TARURA Wilaya ya Arusha, Mhandisi Godfrey Bwire alisema mradi huo umegharimu kiasi cha sh, bilioni 1.7 ikiwa ni mapato ya ndani ya halmashauri ya Jiji la Arusha.
Bwire ameeleza kuwa gharama hizo zinajumuisha miundombinu ya umeme, maji taka na maji safi, ujenzi wa barabara kwa kiwango cha zege, uwekaji wa alama za barabarani pamoja na ujenzi wa mitaro Maboresho ya mifereji ya maji ni sehemu muhimu ya jitihada za kupunguza athari za mafuriko katika maeneo ya Sakina na vitongoji vinavyozunguka.
Alisema mradi nuo unatekeiezwa na kampunΔ± ya Jiangxi Geo-Engineering (Group) Corporation ulioanza kutekelezwa Juni 1,2026 na kukamilika Oktoba 28 mwaka huu Wakati huo huo.
Kwa upande wake Mbunge wa viti maalum Mhe. Marirta Gido, ameeleza kuwa kwasasa jiji la Arusha linaendelea kuwa kivutio kikubwa hasa katika maswala ya utalii na kuelekea katika maahindano ya Afcon 2027 hivyo ni vyema miundombinu kutunzwa na kulindwa.
"Tunamshukuru Rais Dkt. Samaia kwa kuendelea kuwekeza katika miradi ya wananchi na kuendelea kutatua kero ambazo zinaweza kupunguza uchumi wa taifa letu, lakini tukiwa na miundo mbinu salama ni rahisi itachochea kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi kwa wananchi". Amesema Gido.
"Barabara hii ya Giriki imekuwa miongoni mwa mahitaji makubwa ya wananchi wa Kata ya Sakina kwa muda mrefu kupitia barabara hiyo muhimu itaongeza usafiri, biashara na maendeleo ya eneo hili". Ameongeza Gido.
"Kipekee, moyo wangu umejaa shukrani. Napenda kuendelea kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuleta fedha za utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo" Amesisitiza Gido.
Naye Diwani wa Kata ya Sakina Hillar Mollel ameeleza kuwa barabara hiyo inaenda kuwa chachu kwa wananchi katika ukuaji kiuchumi kwa wananchi maana imekomeshwa katika kipindi cha mvua za masika.
"Serikali imeendelea kutekeleza miradi hasa katika kufungua njia za mzunguko katika Jiji la Arusha hasa katika swala zima la uwekezaji,kikubwa tunamuomba mkandarasi amalize mradi kwa wakati iki wananchi waendelee kutumia barabara hii na kuweza kupata mafufaa kwa maendeleo ya kiuchumi". Amesema Mollel.
Comments
Post a Comment