MWANAFUNZI ALIA NA MWALIMU MKUU ADAI ALIWAMBIA HAKUNA KUSEMA POPOTE.
KAULI TOKA OFISI YA MBUNGE JIMBO LA CHALINZE
Kupitia malalamiko ya Mwanafunzi huyo muhitimu wa darasa la saba kutoka shule ya Chalinze Modern aliye fahamika kwa jina la Iptosum Suleman Silm kubadilishiwa namba yake ya kufanyia mtiahani kutoka namba 39 aliyosajiliwa nayo hadi kufanya mtihani kwa namba 40 ambayo hakusajiliwa nayo.
Malalamiko hayo ambayo yamekuwa yakienea kwa kasi sana kupitia mitandao ya kijamiii kutoka kwa wanaharakati na wapenda maendeleo ya taifa letu la Tanzania hatimaue yamefika kqtika uongozi wa Jimbo la Chalinze kuoitia Mbungu wa Jimbo hilo hilo Mhe, Ridhiwani Kikwete ambaye pia ni Naibu Wazriri wa Wizara ya Ardhi, Nymba na maendeleo ya makazi.
"Nimepokea taarifa zinazomuhusu Binti yetu anayeitwa Iptosum Suleiman Slim kuhusu shida iliyotokea kwenye Mitihani yake ya Darasa la Saa katika shule ya Msingi ya Chalinze Modern. Binafsi nieleze kwanza masikitiko kwa tukio zima maana linatupa nafasi ya kuhoji juu ya ukweli wa habari nzima, Si jema kwa Mwanafunzi, Shule wala Halmashauri yetu ya Chalinze". Alieleza Ridhiwani.
"Nimeuelekeza Uongozi wa Halmashauri yetu na Shule kutafuta jawabu ya changamoto hii. Nimewataka kuhakikiaha jamii inapatiwa taarifa za ukweli kuhusu tukio zima na kama itakuwa kuna yeyote aliyehusika kuweka mazingira haya ikiwa ni dhuruma kwa mwanafunzi wetu huyu au kuchafua sura ya Shule yetu basi hatua za msingi kupata haki zifuate". Aliongeza Ridhiwani.
"Elimu ni kipaumbele chetu,kusomesha watoto wa kike ndiyo njia ya ukombozi wetu. Ninaamini Halmashauri yetu yenye wajibu wa kusimamia Elimu watatoa taarifa punde kama nilivyoelekeza,
Tunaomba Utulivu wakati jambo hili linafanyiwa kazi hili tupate muafaka wake. Ninaamini Haki itatendek kwa pande zote zinazohusika". Alisisitiza Ridhiwan.
Aidha katika Clip fupi ya daki takribani 4 zinamuonyesha binti huyo akiomba msaada kutoka mamlaka husika baada kutokuona alicho ahidiwa na msimamizi wake wa mtihani kutokufanyiwa kazi maana alihaidiwa watafatilia tamisemi na kuweka sawa.
Katika Malalamiko hayo Binti Iptosum anasema yeya alisajikiwa na Kufanya mtihani wa darasa la saba kwa usaili wa namba ya shule ya Chalinze Modern kwa namba 39 lakini ilipo fika siku ya mtihani aliingia katika chumba cha mtihani ailiambiwa namba yake ni 40 kitu ambacho kilimshangaza lakini msimamizi alimuelekeza afanye tu kwa namba hiyo 40 na atafuatilia ili kujua tatizo ni nini.
Iptosum anaendelea kueleza kuwa aliweza kufanya mitihani 5 kwa namba hiyo 40 lakini ilipofika mtihani wa mwisho wa aliamuliwa afanye mtihani huo kwa namba yake halisi namba 39 mtiani ambao anaeleza kwake hauna mashiko maana ni wasanaa sasa malala miko yake zaidi ni ni juu ya mitihani yake 5 ambayo niyamuhimu.
Aidha binti huyo anaomba asaidiwe kisheria kupitia baraza la mitihani hapa mchini ikiwemo wizara ya elimu pamoja na wizara ya Tamisemi maana anaeleza baada ua tukio hilo waliitwa na Mwalimu wao Mkuu akimtaja kwa jina la Kijangwa na kuambiwa wasieleze chochote kwa wazazi wao wala kwa mtu yeyote.
"Kiukweli ninaomba nisaidiwe kisheria kupitia baraza la mitihani,watangazaji na wanasheria ili nipate matokeo yangu kwa nanga yangu halisi maana namba hiyo 40 niliyopewa kufanyia mtihani huyo mwenye namba hiyo 40 huwa anakuwa wa mwishoni darasani naona ndiyo maana nikapewa namba yake na mimi huwa nakuwa 10 bora". alisema binti huyo.
Hapo wasi wasi mkubwa wa binti huyo ni pale mwalimu mkuu alivyo waita wachache na kuwapa onyo la kutokusema wenda hao wote wamechezewa mchezo huo huo wa kuwafanyia wenzao wasio jiweza darasani.
Hapa ni wazi mamlaka husika zianze kuchukua hatua za haraka kuinusuru shule hiyo na kutenda haki kwa wanafunzi hao ambao hadi sasa hajui hatima yao.
Endelea kutufuatilia kupitia mitandao yetu mingine ya kijamii ikiwemo Twitter,Youtube & Instagrame
Kwa mawasiliano zaidi 0763 420 108
Comments
Post a Comment