BONANZA KUBWA KUELEKEA MIAKA 5 YA MATI SUPER BRANDS LTD LATIKISA

Na Lucas Myovela_ Manyara 


BONANZA LA MIAKA 5 YA KAMPUNI YA MATI SUPER BRANDS LIMITED LAFANA. 


Wafanyakazi wa kampuni ya Mati Super Brands Limited wameshiriki katika bonanza Maalumu kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Miaka 5 ya kuanzishwa kwa kampuni ya Mati Super Brands Limited iliyoko mkoani Manyara. 

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mati Super Brands Limited David Mulokozi amesema kuwa bonanza hilo limehusisha michezo mbali mbali ikiwemo mpira wa miguu,kuvuta kamba n.k. 

Mulokozi amesema kuwa lengo la bonanza hilo ni kudumisha umoja na mshikamano wa wafanyakazi wa kampuni hiyo ambao wamefanya kazi kwa weledi kwa kipindi cha miaka 5


Afisa Rasilimali watu Wa kampuni ya Mati Super Brands Limited Doreen Raphael amesema kuwa kila mwaka kampuni hiyo inaajiri wafanyakazi wengi hivyo ni michezo hiyo inatoa fursa kwa wafanyakazi kufahamiana na kudumisha umoja unaoleta tija mahala pa Kazi. 

Kwa upande wake Mwakilishi wa Wafanyakazi wa  kampuni ya Mati Super Brands Limited amepongeza uongozi wa kampuni hiyo kwa kuja na mawazo ya ubunifu wa kujenga umoja na mshikamano kupitia michezo.

Comments