MATI SUPER BRANDS YAHIMIZA MICHEZO VIWANDANI:

KAMPUNI YA MATI SUPER BRANDS YACHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA BONITE BOTTLERS  LTD MANYARA. 

 Na Lucas Myovela _ Manyara.


Kampuni ya Mati Super Brands Limited imecheza mechi ya kirafiki na kampuni ya Bonite bottlers Ltd katika viwanja vya Kwaraa Wilayani Babati Mkoani Manyara  ikiwa ni njia mojawapo ya kukuza vipaji vya soka pamoja na kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwa kampuni hizo zinazoshiriki katika masuala mbali mbali ya kijamii na kuchangia maendeleo ya Mkoa wa Manyara na taifa kwa ujumla. 


Meneja Masoko wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited Elvis Peter amesema kuwa mechi hiyo ni muendelezo wa kampuni hiyo kushirikiana na makampuni yaliyoko mkoani Hapa pamoja na kujenga ujirani mwema. 

Elvis amepongeza uongozi wa Mati Super Brands Limited pamoja na Bonite Bottlers ltd kwa kutoa fursa kwa wafanyakazi wao kushiriki katika michezo ya pamoja ambayo inasaidia kukuza vipaji na kuimarisha afya za miili yao ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi na kuzalisha kwa tija. 


Nahodha wa Timu ya Bonite Bottlers limited Maboya Ramadhan ameeleza kufurahishwa na mchezo huo uliogubikwa na ushindani mkubwa ,na kuzitaka taasisi nyingine kuiga mfano na kuhimiza michezo kwa wafanyakazi. 


Maboya ameendelea kusema kuwa Bonite wamekua mstari wa mbele katika kuibua vipaji vya soka kwa vijana  na kutoa fursa kwa vijana kujiendeleza kimichezo.

Comments