WAZIRI KIKWETE ASHIRIKI WIKI YA UTUMISHI AFRIKA NCHINI ZIMBABWE.⁷

NAIBU WAZIRI WA UTUMISHI NA UTAWALA BORA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI AFRIKA, ZIMBABWE.

Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Ndg. Ridhiwani Kikwete ameshiriki shughuli ya Utumishi wa Umma Afrika zilizofanyika Katika Jiji la Victoria Falls nchini Zimbabwe.

Sherehe hizo ambazo uzikutanisha nchi zote wananchama wa Jumuiya ya Afrika zilifanyika zikiwa na ujumbe kuwa mafanikio ya ukuzaji Biashara eneo huru la Biashara Afrika ni hitaji la Utumishi wenye Tija kufanikiwa.


Katika mkutano huo ujumbe wa Tanzania ulitolewa na Naibu Waziri Kikwete , ambapo ameeleza mafanikio yaliyofikiwa na  Serikali ya awamu ya Sita chi ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassa huku Uongozi wa Nchi yakichagizwa na mabadiliko ya kimfumo na kiutendaji yaliyofanywa katika Utumishi wa Umma.

Akieleza Naibu Waziri Ndg. Kikwete,  alieleza mabadiliko katika mfumo wa utendaji kazi na utambuzi yaani PEPMIS, PIPMIS na HCMIS ni baadhi ya hatua kubwa kuleta uwajibikaji kazini.


Pamoja na hayo miundombinu inayojengwa ikiwemo Great EA Road inaunga Kenya na Tanzania kwenye kusini na Kaskazini mwa Afrika , Uwekezaji Bandari Ya Dsm,Reli ya Kisasa (SGR), mabadiliko ya Shirika la Ndege -ATC.

Ujenzi wa Vituo vya Biashara vya Pamoja Mipakani na Mradi mkubwa wa Umeme ni alama za mabadiliko makubwa yatakayowezesha Biashara kufanyika vzr na kwa kasi katika eneo la Mashariki na Afrika kwa jumla.


Hata hivyo Mkutano Mkuu ujao wa Utumishi Afrika utafanyika Nchini Ethiopia, Mwaka 2025.

Comments