WANANCHI MIRERANI WAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUMPA MUWEKEZAJI MZAWA KITALU C, WAOMBA AENDELEE KULINDWA DHIDI YA WACHIMBAJI WENGINE WANAO VUNJA SHERIA ZA UCHIMBAJI.
WAMSHUKURU RAIS SAMIA KUWAJALI WAZAWA NA KUWAPA NAFASI YA KUJENGENGA TAIFA KWA PAMOJA KATIKA KUKUZA UCHUMI.
Na Lucas Myovela_ Mirerani.
Wafanyakazi wa Kampuni ya wawekezaji wazawa hapa nchini kupitia kampuni ya uchimbani wa Madini ya Tanzanite ya Franone Mining and Games Campany LTD, inayochimba Madini ya Tanzanite katika Kitalu C katika Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara wamempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wawekezaji wazawa hadi kupelekea wao kupata ajira tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Wakizungumza kwenye mgodi huo na vyombo vya habari wamemshukuru mwekezaji huyo kwa kuwapatia ajira pasipo masharti yeyote magumu tofauti na awali ambapo hawakuwa na kazi ya kufanya kwa ajili ya kuwapatia kipato lakini sasa hivi wamekuwa na uhakika wakujipatia kipato kinachotokana na kazi hiyo ya ufumaji wa mifuko maalumu pamoja na kamba zinazo tumika mgodini hapo.
Kwa upande wake kiongozi wa kikundi cha akina mama wanaofanya kazi katika kampuni hiyo Bi Nai leyani, Amesema serikali iendelee kumlinda mwekezaji huyo na kuwapa elimu wachimbaji wadogo ili kuondokana na tatizo la mitobozano ambayo imekuwa ni kero kwa mwekezaji kwa sababu wapo watu wanaoamini kuwa kitalu C peke yake ndiyo kinamadini.
Alisema pasipo serikali kuangalia kwa jicho tatu mwekezaji hatoweza kuendelea na shughuli kwa sababu wachimbaji wadogo wanadaiwa kuendelea kuchimba kuelekea kwenye kitovu cha Kitalu c,"alisema Nai.
Naye Joram Madole mwakilishi wa Wazee walionufaika na uwekezaji huo amesema awali wakati wa mwekezaji Mzungu walikuwa hawawezi kuingia kufanyakazi lakini sasa hivi wanafanyakazi kwa amani na utulivu na wanajipatia kipato cha kuwasomeshea wajukuu zao.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo,Vitus Ndakize alisema kampuni hiyo imeweza kutoa ajira rasmi 386 na ajira 1000 ambazo siyo rasmi ambao ni wachekechaji na kazi yao kubwa ni kuchekecha udongo ambao unatoka chini ya mgodi na kwa kufanya hivyo wanajipatia riziki zao.
Ndqkize alisema kupitia mgodi huo wameendalea kushirikiana na jamii inayowazunguka kwa kuchangia michango mbalimbali ikiwemo ukarabati wa Barabara kiwango cha changalawe kutoka getini hadi mgodini hapo.
Pia aliongeza kuwa wanatoa chakula katika shule mbili za Sekondari ambazo ni Mirerani, na Naisinyai kwa sababu kulikuwa na ukosefu wa mvua uliopelekea shule hizo kukosa chakula hivyo waliguswa na waliweza kutoa chakula cha mwaka mzima na kutoa madawati 100 katika shule ya Mirerani.
Katika hatua nyingine,Vitus Ndakize alisema Mgodi huo umekuwa na changamoto kubwa ya mitobozano kutokana na uelewa mdogo wa wachimbaji wadogo na kwakuwa mikondo ya Tanzanite imelala kuanzia Kitalu A,B inapita Kitalu C na inaenda D mpaka D Extensioni na huko kote madini yapo na huo ndiyo uelekeo wa madini hayo.
"Watu wengi wanaamini kuwa madini yapo kitalu C na si kwamba yapo kitalu C peke yake ni kwa sababu kitalu kilifanyiwa tafiti za kutosha hivyo kinaweza kuwa na uzalishaji endelevu kwa sababu hivyo vitalu vingine havina tafiti za kutosha kwa maana hiyo watu wanachimba kwa kubahatisha". alisema Ndakize .
"Mitobozano inaweza ikaleta maafa makubwa kwa kuuwa watu kwa sababu kule chini kazi za ulipuaji zinapofanyika na kinachofanya kazi ni baruti na inapotokea kuna mtu anaripua pasipo kuwa na taarifa watu wanaweza kujeruhiwa". alisema Ndakize.
Alisisitiza ili kumaliza tatizo la mitobozano Serikali lazima iendelee kutoa elimu ya mipaka ya maeneo yao kwa sababu
wapo baadhi ya wachimbaji bado wanaamini chini ya ardhi hakuna mipaka jambo ambalo siyo kweli.
Comments
Post a Comment