RC MAKONDA ATAKA ONGEZEKO LA THAMANI KWENYE BIDHAA ZA KILIMO.

ATAKA VIWANDA VYA KUONGEZA THAMANI YA MAZAO ILI KUWA NA TIJA NA FAIDA KWA WAKULIMA.

MWENYEKITI WA HALMASHAURI HIYO ALIPOKEA NA KUAHIDI KULIFANYIA KAZI KWA WAKATI NA UKARIBU ZAIDI.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru kubuni mpango wa kuwezesha ujenzi wa viwanda vya kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo ili kuongeza tija kwa wakulima na wafugaji wanaopatikana wilayani humo.


Mkuu wa Mkoa ametoa kauli hiyo leo wakati alipofika kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha na kuzungumza na watendaji wa Wilaya hiyo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya Kikazi ya kutembelea Wilaya zote sita za mkoa wa Arusha.

Mhe. Makonda amewaambia watumishi wa Halmashauri hiyo kuwa sifa kuu ya Kiongozi inapaswa kuwa ya kuwaondoa wananchi kwenye umaskini na kuwapa fursa nyingi zaidi za kuweza kujishughulisha na uzalishaji mali kwa maslahi yao binafsi na ya Taifa.


Akitilia mkazo suala lake hilo Mhe. Mkuu wa Mkoa ameiagiza Halmashauri hiyo pia kutafuta mazao ya kimkakati yatakayoitambulisha wilaya hiyo akishauri nguvu kuwekezwa kwenye kilimo cha mazao yanayotumika kwenye kutengeneza marashi kwani tafiti zinaonesha kuwa ardhi ya Wilaya ya Arumeru inafaa kwa kilimo hicho.

Katika mazungumzo yake na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw. Jeremia Kishili, Mhe. Mkuu wa Mkoa pia ameagiza kuundwa kwa mkakati maalum wa kuvutia sekta na watu binafsi kuwekeza kwenye nyumba za kulala wageni na watalii mbalimbali hasa kwa wale wanaotumia uwanja wa ndege wa Kilimanjaro kuingia nchini Tanzania.


Comments