JIJI LA ARUSHA LAFIKIWA, WATAKIWA KUWA KINARA KATIKA KUPIGA KURA KATIKA UCHAGUZI WA VIONGOZI SERIKALI ZA MITAA.

MKURUGENZI KAYOMBO AFUNGUKA YOTE KWA WANANCHI WA JIJI LA ARUSHA KUANZIA KESHO.


WANANCHI MKOANI ARUSHA WATAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUJIANDIKISHA KWENYE ORODHA YA WAPIGAKURA KESHO.

Na Lucas Myovela - Arusha.


Wananchi wote Mkoani Arusha wametakiwa kujitokeza kwa wingi kesho oktoba 11 kujiandikisha kwenye daftari la orodha la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa ili waweze kupata haki ya kupiga kura siku ya uchaguzi. 
Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake, Mkurugenzi wa jiji la Arusha ambaye ni Msimamizi wa uchaguzi,John Kayombo amesema kuwa ,maandalizi yote yamekamilika na kuwa uandikishaji utaanza kesho oktoba 11 na utaendelea hadi oktoba 20,kuanzia saa mbili hadi saa kumi na mbili jioni. 


 "Kwa upande wetu tumeisha kamilisha maandalizi yote ya zoezi la uandikishaji na tumewakumbusha wadau wa uchaguzi ambao ni vyama vya siasa kuweka mawakala katika vituo vya uandikishaji na wahakikishe mawakala hao wameapishwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa Wenyeviti wa mtaa na wajumbe wa kamati ya mtaa katika mamlaka za miji za mwaka 2024."amesema .


 Ameongeza kuwa, tangazo la serikali namba 574 la mwaka 2024 nakala za viapo zimetolewa kwa viongozi wa vyama ili kuwarahisishia mchakato wa kuapisha mawakala .


 Amefafanua kuwa ,orodha ya vituo vyote vya kujiandikisha kwa vyama vya siasa na upangaji wa vituo umezingatia azma ya kupunguza foleni ili kuruhusu watu kujiandikisha kwa wepesi na kuendelea na shughuli zao za uzalishaji Mali.


Aidha Kayombo amewataka wananchi kutambua kuwa uchaguzi huu ni muhimu sana kwani wanakwenda kuchagua viongozi watakaoshughulika na mambo ya wananchi na maisha yao ya kila siku. 


 "Nawaomba pia viongozi wa vyama vya siasa tuendelee kushirikiana katika hatua zote na endapo kiongozi yeyote wa chama atahisi kuna changamoto yoyote katika zoezi la uandikishaji awasiliane na ofisi ya msimamizi wa uchaguzi."amesema Kayombo.

Comments