TCRA WAZINDUA KAMPENI YA ULINZI MITANDAONI. MATAPELI WAJIPANGE KUSHIKWA WAKATI WOWOTE.

WATANZANIA SASA KULIDWA KIUSALAMA MTANDAONI DHIDI YA WAHALIFU WA KIMTANDAO WANAO WALAGHAI. 
Na Lucas Myvela-Arusha


NUKUU: "Watu wengi nchini hawana ujuzi wa kutosha wa matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii pamoja na namna ya kulinda usalama wao mtandaoni jambo linalowafanya kuwa hatarini kwa mashambulizi ,ulaghai wa mtandaoni na pia matumizzi mabaya ya mitandao ya kijamii".

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Kaskazini imeanzisha kampeni ya kuwahimiza watanzania kujilinda dhidi ya uhalifu mtandaoni kwani uwepo wa mazingira salama mtandaoni utawezesha kufikia malengo ya uchumi wa Kidijiti.

Hayo yameeleza leo Oktoba 09,2024 Jijini Arusha na Meneja wa TCRA Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Francis Mihayo wakati  akiongea na waandishi wa habari na kusema kuwa katika wakati wa sasa wa kidigitali matumizi ya teknolojia yamekua yakiongezeka kwa kasi na ni muhimu sana katika maisha ya kila siku hivyo ni wajibu wa Mamlaka hiyo kutoa elimu ya matumizi bora ya mitandao kwa watanzania.


"Watu wengi nchini hawana ujuzi wa kutosha wa matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii pamoja na namna ya kulinda usalama wao mtandaoni jambo linalowafanya kuwa hatarini kwa mashambulizi ,ulaghai wa mtandaoni na pia matumizzi mabaya ya mitandao ya kijamii". Amesema Eng. Mihayo.


"kufuatia hali hiyo TCRA kupitia kitengo cha mawasiliano na mahusiano ya Umma (CPRU) inatambua umuhimu wa kukuza elimu ya kidigitali na kuhamashisha juu ya fursa zilizopo kwa matumizi sahihi mtandao kwa wananchi wote kushiriki kwa usalama kiuchumi na kisiasa hasa katika kipindi cha chaguzi mbalimbali nchini". Ameongeza Eng. Mihayo.

Mhandisi Mihayo ameeleza kuwa TCRA inaungana na Dunia katika kuadhimisha mwezi wa elimu ya usalama mtandaoni ambayo huadhimishwa kila mwaka mwezi octoba na kitaifa ilizinduliwa Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt Jabir Bakari kwa uzinduzi kabambe uliojulikana kwa jina la ‘’Ni rahisi sana’’ na kwa kanda ya kaskazini imezinduliwa jana na meneja wa Mamlaka hiyo.


Alisema katika kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ujao watanzania wanapaswa kuwa makini na taarifa za mitandaoni kwani baadhi ya watu watatumia mitandao hiyo kutoa taarifa feki na kuzua taharuki hivyo wanapaswa kuwa makini na hilo ili kujiepusha na hilo.


Meneja huyo alisema TCRA imekuwa ikitoa elimu katika maeneo mbalimbali ya wazi kwa miaka mingi ingawa utoaji wa elimu umeendelea kuwa endelevu wakati wote na mabadiliko ya kasi ya teknolojia yamekua yakienda sambamba na ongezeko la vitendo vya ulaghai mitandaoni,ambapo wahusika wamekua wakibuni mbinu mpya kila wakati na kusababisha elimu ya usalama iwe endelevu.


Alisema kampeni hiyo ina lenga kuwapa watu maarifa muhimu ya kidijitali yanayohusu usalama mtandaoni,kuongeza uelewa juu ya jinsi TCRA inavyosaidia bunifu mbalimbali zinazohusu TEHAMA,kuongeza uelewa juu ya kuripoti vitendo vya ulaghai na kukomesha kueneza habari za uongo kwa jamii na kuthamini wateja na wadau wengine nchini.

Comments