WAZIRI ULEGA AWAONYA VIKALI WASIMAMIZI WA MIRADI NAWAKANDARASI, ASEMA DKT. SAMIA AWAPA KIPAUMBELE WAKANDARASI WAZAWA.
🔺️WANAO CHELEWESHA MIRADI YA BARABARA KUKIONA CHA MOTO ULEGA AGEUKA MBOGO.
🔺️ATEMBELEA UJENZI WA DARAJA LA KING'ORI WILAYA YA ARUMERU, AIPONGEZA TANROAD'S ARUSHA.
Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi imetekeleza jumla ya miradi 81 ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu yenye thamani ya shilingi Bilioni 500, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, ndani ya siku 100 katika sekta ya miundombinu ya barabara nchini, ambapo wizara imejipanganga kuboresha miundombinu kuanzia vijijini hadi Mijini.Amesema kuwa, mradi huo wa daraja unahusisha uwekaji wa taa 136 za barabarani kwenye barabara hiyo kutoa uwanja wa ndege wa Kimataifa Kilimanjati (KIA) mpaka Jiji la Arusha jambo ambalo litaonheza usalama wa watumiaji wa barabra hiyo hasa nyakati za usiku.
Waziri Ulega,amezungumzia changamoto ya baadhi ya Wakandarasi kutoka nje ya nchi kukwamisha utekelezaji wa miradi, hali iliyosababisha wizara kushirikiana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kubaini vipengele vya kisheria vinavyokiukwa, na endapo itabainika kuna uzembe, Serikali itavunja mikataba hiyo.
"Natoa onyo kwa wasimamizi wa miradi na wakandarasi wanaosababisha ucheleweshaji wa miradi ya barabara kwamba hatutasita kuchukua hatua kali, hasa katika Mkoa wa Kagera ambako shilingi bilioni 9 zilitolewa kwa ajili ya ujenzi wa barabara lakini hakuna utekelezaji unaoonekana," Amesema Ulega.
Ameongeza kuwa, kazi zote za zabuni zenye thamani isiyozidi shilingi billioni 50 hazitaruhusiwa kupewa wakandarasi wa kigeni, zitatekelezwa na wakandarasi wazawa. na mingine italazimika kutekelezwa kwa kushirikiana wakandarasi wa nja na wazawa kwa asilimia 10 ili kuwaongezea ujuzi.
Aidha ameeleza kuwa Wizara yake imejipanga ipasavyo kuhakikisha barabara zote zinapitika kuanzia vijijini hadi mijini lengo likiwa ni kusogeza huduma kwa jamii kwa kuwa na miundombinu inayofikakika kikamilifu pasipo vikwazo kitu ambacho kitachochea ukuaji wa uchumi kwa wananchi.
Amesema Miundombinu ikiwa bora ni rahisi wananchi kufanya safari zao pasipo vikwazo na Serikali imejipanga katika hilo ili kuweza kutoa fursa kwa wananchi kusafirisha mazao yao au kufanya biashara pasipo vikwazo vya kiundombinu.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Dk. Charles Msondo, amesema siku 100 za uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, zimeleta tija kwa wananchi na kuchangia kuinua uchumi wa taifa.
Mwinyi ameeleza kuwa daraja hilo limetatua adha kubwa kwa wananchi hasa kipindi cha mvua za masika maji kuwa mengi na kushababisha hata wakati mwingine magari kutokuoita kutokana na daraja lililo kuwepo awali kuwa ni dogo.
Kwa upande wake M'bunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshia Nassari, ameishukuru Serikali kwa kutatatua changamoto hiyo ya daraja hilo na kuwapongeza TANROAD'S Mkoa wa Arusha kwa kusimamia vizuri mradi huo ambao umegusa maisha ya watanzania wengi hasa kwa wasafiri ambao wanatumia barabara hiyo.
Amesema Siku 100 za Dkt. Samia zimekuwa chachu kwa wananchi wa Meru kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika nyanja mbalimbali ikiwemo miundombinu, elimu, afya n.k.










Comments
Post a Comment