WAZIRI OMAR AKIPONGEZA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA KWA KUFANYA MAGEUZI YA KIDIGITALI PAMOJA NA UFANYAJI TAFITI KUFIKIA DIRA YA TAIFA 2050.

🔺️2250 WAHITIMU SHADA YA UZAMILI TAYARI KULITUMIKA TAIFA KATIKA FANI MBALIMBALI NA WENYE KUKIDHI SOKO LA AJIRA NDANI NA NJE YA NCHI.

Na Lucas Myovela - Arusha.

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, amekipongeza Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kwa kufanya mageuzi makubwa ya kidigitali, ufanyaji wa tafiti, maendeleo pamoja na mipango na mikakati ya kuboresha na kuongeza ufanisi kwenye utoaji wa mafunzo na ushauri wa kitaalam, ambazo ni miongoni mwa vichocheo vya kufikia Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025-2050.

Hayo yasemwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula, wakati akihutubia kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mh. Balozi Khamis Mussa Omar, katika Mahafali ya 27 (Duru ya Pili) ya Chuo hicho, yaliyofanyika katika Hoteli ya Ngurdoto Mkoani Arusha.


Luswetula amesema kuwa mchango wa chuo cha IAA katika uchumi wa Taifa ni mkubwa kwa kuwa kimeendelea kuzalisha wataalam wa fedha, uhasibu uchumi, kodi, utalii, usimamizi biashara ya benki, ununuzi na ugavi, masoko, bima, TEHAMA na nyingine nyingi.


"Matumizi ya mfumo wa ana kwa ana darasani sambamba na mfumo wa mtandaoni (online), Mfumo huu umeongeza upatikanaji wa elimu, kuboresha ubora wa ufundishaji, na kuwapa wanafunzi unyumbufu unaoendana na mazingira ya kazi na maendeleo ya teknolojia ya kisasa, Huu ni ushahidi wa wazi kuwa Chuo kinaendana na mabadiliko ya dunia ya sayansi na teknolojia". Amesema Luswetula.


Ameeleza kuwa Wataalam hao wamekuwa mhimili muhimu katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali, usimamizi wa fedha za umma, sekta binafsi, taasisi za kifedha na miradi ya maendeleo na Kupitia wahitimu wake Chuo hicho kimechangia kwa vitendo katika kukuza uwajibikaji, uwazi na nidhamu ya kifedha hapa nchini.


"Niwapongeze IAA mmeendelea kudhihirisha umahiri mkubwa katika kuandaa rasilimali watu mahiri, wanaokidhi mahitaji ya soko la ajira ndani ya nchi na nje ya nchi na kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya uchumi wa Taifa letu"Amesema Luswetula.


Aidha Luswetula, ameupongeza uongozi wa Chuo cha lAA kwa kuwa kinara katika kuboresha mifumo ya ufundishaji na ujifunzaji kupitia matumizi ya teknolojia za kisasa sambamba na kuimarisha tafiti na ushauri wa kitaalam.

"IAA imeendelea kuzalisha wataalam wa fedha, uhasibu, uchumi, kodi, utalii, usimamizi biashara, benki, ununuzi na ugavi, masoko, bima, TEHAMA na nyingine nyingi ambao imeleta Mageuzi ya kidigitali ni kichocheo muhimu cha maendeleo hususan katika kuboresha ukuaji wa uchumi na kuimarisha huduma za jamii ikiwemo elimu". Amesema Luswetula.


"Serikali inatambua na kupongeza juhudi za IAA katika kuwekeza kwenye mifumo ya kidigitali na katika kuimarisha ufanisi wa utoaji wa elimu kwa njia bunifu," aliongeza Mhe. Luswetula.


Pia Luswetula ameeleza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na vyuo vya elimu ya juu, ikiwemo IAA, ili mitaala iendelee na kuendana na mahitaji halisi ya soko la ajira na mabadiliko ya uchumi wa kidijitali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi wa Chuo hicho Dkt. Mwamini Tulli, ameeleza kuwa chuo cha IAA kimejipanga kuendelea kutoa wahitimu mahiri kwa kuwekeza katika rasilimali watu, hususani wahadhiri wenye sifa, uzoefu wa kitaaluma na kitaalam, pamoja na kuimarisha mbinu shirikishi za ufundishaji na ujifunzaji.


Ameeleza kuwa Ubora huo wa elimu wanao utoa unatokana na mitaala inayozingatia mahitaji ya sasa ya soko la ajira, maendeleo ya teknolojia, na mabadiliko ya kiuchumi na kijamii.


"Mipango na maendeleo ya Chuo imejikita katika upanuzi wa programu za Uzamili, uanzishwaji wa kozi mpya zinazokidhi mahitaji ya soko, pamoja na kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji, ujifunzaji na usimamizi na Kupitia programu zetu za Shahada ya Uzamili, Chuo kitaendelea kujikita katika kuandaa viongozi, wasimamizi na wataalam wenye uwezo wa kufanya maamuzi sahihi, kuzingatia misingi ya uwajibikaji, uwazi na utawala bora". Amesema Dkt. Tulli.

Naye Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha IAA Pof. Eliamani Sedoyeka ameeleza kuwa Jumla ya Wahitimu wanaohitimu ni 2,250 kati yao wanaume ni 1,369 sawa na asilimia 60.8% na wanawake ni 881 sawa na asilimia 39.2% katika shahada ya uzamili katika fani mbalimbali na wakiwa tayari kwenda kulitumikia taifa.


"Kama Chuo tumejiwekea vipambele ambavyo vitakuwa chachu ya ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yetu ya msingi kama taasisi ya elimu ya juu ya kutoa mafunzo, kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalam, Vipaumbele vyetu ni Kuwekeza kwenye Mitaala inayoendana na mahitaji ya wakati ya soko la ajira". Amesema Prof. Sedoyeka.


"Kuwekeza katika kuimarisha rasilimali watu, Kuwekeza katika kuboresha miundombinu ya kujifunzia na kufundishia, Kuwekeza katika kuongeza vyanzo vipya vya mapato zaidi ya ada za wanafunzi, Kuwekeza zaidi katika mipango na mikakati ya umataifishaji (Internationalization), Kuwekeza katika ujenzi na uboreshaji wa miundombinu na huduma za TEHAMA". Ameongeza Prof. Sedoyeka.


Amesema kwa kutambua mabadiliko ya kasi katika mahitaji ya soko la ajira na uongozi wa kitaifa, Chuo hicho kinaendelea kuimarisha huduma za ufundishaji na ujifunzaji kwa kuboresha mitaala, mbinu za kufundishia, na mifumo ya tathmini ili kuendana na sera, mikakati, na dira ya maendeleo ya Taifa.


"Mmeandaliwa kuwa viongozi wenye maarifa, maadili, na uwezo wa kuongoza mabadiliko chanya katika taasisi na jamii mnayoihudumia. Matarajio yetu ni kwamba, mtazingatia misingi ya uwajibikaji, uadilifu, na uzalendo katika kutekeleza majukumu yenu ya kitaaluma na kitaifa". Amesema Prof. Sedoyeka.






















Comments