HII NI ZAIDI YA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA ELIMU NA UCHUMI WA VIWANDA NA KUANDAA KIZAZI CHA WATAALAMU WATAKAO SHINDANA KIMATAIFA KATIKA NYANJA YA TEKNOLOJIA YA KIHANDISI.
Katika hafla ya kuwaaga walimu hao Machi 26, 2026 jijini Dar es Salaam, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesisitiza kuwa mpango wa mafunzo hayo ni utekelezaji wa sera ya elimu ya lazima ya miaka 10, unaolenga kujenga umahiri wa ufundishaji na kuandaa kizazi cha wataalamu wenye ushindani wa kimataifa. Ameeleza kuwa safari ya mageuzi ya elimu inaendelea na haitarudi nyuma, huku akiwataka walimu watambue nafasi yao kama daraja kati ya sera na utekelezaji darasani.
Kamishna wa Elimu Dkt. Lyabwene Mtahabwa ameeleza kuwa mafunzo hayo ya mwezi mmoja yamewahusisha walimu kutoka mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na viongozi wa ngazi ya elimu mkoa kutoka mikoa tisa ili kusimamia kikamilifu uendelevu wa mafunzo warudipo nchini.
Wanufaika wa mafunzo hayo, akiwemo Mwalimu Judith Faustine wa Uhandisi Ujenzi katika Shule ya Sekondari Mwadui Ufundi na Mwalimu Jacob Mwalyego wa fani ya Uashi katika Shule ya Sekondari ya Ufundi Mbogwe, wameishukuru Serikali kwa kuwapatia nafasi hii ya kipekee. Wamesema ni heshima kubwa na fursa ya kuongeza maarifa yatakayowawezesha kuendeleza mageuzi ya elimu nchini.






.jpg)









Comments
Post a Comment