đź’˘YAPANGA KUFANYA MABORESHO ILI KUWAWEZESHA MAWAKILI WA SERIKALI KUENDANA NA MABADILIKO YA KIUTENDAJI KATIKA UTOAJI HAKI KUELEKEA DIRA YA TAIFA 205O.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Juma Zuberi Homera, amesema Serikali inaendelea kufanya maboresho mbalimbali katika Sekta ya Sheria nchini kwa lengo la kuwawezesha Mawakili wa Serikali kwenda sambamba na mabadiliko ya kiutendaji na mahitaji ya kisasa ya utoaji haki.
Dkt. Homera, Amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia Mawakili wa Serikali kujifunza mbinu za kisasa katika usimamizi wa mashauri ya Serikali, usimamizi wa mikataba pamoja na utatuzi wa migogoro katika sekta mbalimbali.Dkt. Homera amesema hayo wakati akifungua mafunzo maalumu kwa Mawakili wa Serikali Jijini Arusha Mei,18 2026.
Amesema kupitia mafunzo hayo, Mawakili wa Serikali watapata maarifa katika maeneo ya kimkakati ikiwemo usimamizi wa mikataba ya ujenzi na manunuzi, sheria a anga na utatuzi wa migogoro ya anga, sheria za kodi katika sekta ya mafuta na gesi pamoja na uendeshaji wa mashauri katika mabaraza mbalimbali ya utoaji haki."Mada hizi ni mahsusi kabisa katika kufikia lengo la Wizara ya Katiba na Sheria na taasisi zake la maono ya Mageuzi katika Sekta ya Sheria". Amesema Dkt. Homera.
"Mafunzo haya ni sehemu muhimu ya mageuzi katika Sekta ya Sheria nchini na yatawawezesha Mawakili wa Serikali kusimamia vyema mashauri na kuisaidia Serikali kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050," Ameongeza Dkt. Homera.
Aidha, amesisitiza kuwa sheria ni nyenzo muhimu katika kuhakikisha uwepo wa utawala bora, amani, usalama na maendeleo ya kiuchumi, hivyo kuna umuhimu wa kuwa na wataalamu wenye uwezo wa kusimamia masuala ya kisheria kwa weledi mkubwa.
Aidha, Waziri wa Katiba na Sheria ameeleza Mawakiki hao wa Serikali juu ya umuhimu wa maboresho mbalimbali ya Kisheria kwakuwa Sheria ni nyenzo muhimu katika utekelezaji wa Dira ya 2050, ambapo amesema kuwa pamoja na mambo mengine taifa linahitaji watu imara katika kusimamia sheria zitakazoleta amani, utulivu, maendeleo ya kiuchumi kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Vilevile, Dkt. Homera amesema kuwa kuptia mafunzo haya Mawakili wa Serikali wataweza kushauri ipasavyo, kusimamia vizuri mashauri ya Serikali na kuwezesha Serikali Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufikia malengo yake ya DIRA 2050.
"Kama mnavyofahamu kuwa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 imeweka misingi yake katika sekta ya sheria ambayo ni Utawala, Amani, Usalama na Utulivu”. Amesema Dkt. Homera.
Katika hatua nyingine, Dkt. Homera amewasisitiza Mawakili wa Serikali kufuatilia mafunzo hayo kwa utulivu kwani mada hizo zimegusa maeneo muhimu sana katika utekelezaji wa majukumu ya Mawakili wa Serikali.
Kwa upande wake, Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Ally Possi amesema mafunzo hayo yatawasaidia Mawakili wa Serikali kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao kwa viwango vya kitaifa na kimataifa.Dkt. Possi amesema Serikali inahitaji kuwa na jeshi la mawakili wenye maarifa ya kisasa, uwezo wa kutumia teknolojia katika usimamizi wa mashauri pamoja na mbinu za kuzuia migogoro kabla haijafika mahakamani.

















Comments
Post a Comment