đź’˘TANZANIA INABIDHAA ZENYE USHINDANI KIMATAIFA.
đź’˘BODI YA LIGI BORESHENI USIMAMIZI WA MAREFA.
đź’˘WANAHABARI HAMISHENI AJENDA KWENDA KWENYE FURSA ZA KIUCHUMI.
Ameeleza kuwa Tanzania ina bidhaa zenye ushindani mkubwa kimataifa, ikiwemo kakao, parachichi (avocado), tangawizi na mazao mengine ya kilimo, lakini bado hazipewi uzito wa kutosha kwenye vyombo vya habari ili kuvutia masoko na uwekezaji.
Aidha, amebainisha kuwa nchi nyingine zinanufaika na mazao ya Tanzania kwa kuyaongezea thamani (value addition) na kuyauza kimataifa, huku Watanzania wakibaki kwenye uzalishaji wa malighafi bila faida kubwa.
Amesisitiza kuwa vyombo vya habari vina nafasi ya kimkakati katika kuhamasisha uchumi wa viwanda na kuongeza thamani ya bidhaa za ndani kwa kuzielezea, kuzitangaza na kuzifikisha kwenye masoko ya kimataifa.
BODI YA LIGI BORESHENI USIMAMIZI WA MAREFA.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, amewapongeza Watanzania kwa kujitokeza kwa wingi kufuatilia mchezo wa mpira wa miguu uliochezwa Zanzibar, huku akisisitiza umuhimu wa kuboresha viwango vya uamuzi wa marefa nchini.
Amesema licha ya ushindani mzuri uwanjani, bado kuna changamoto katika usimamizi wa marefa, hali inayosababisha mashabiki kupoteza imani na hata kufikia hatua ya kuwasifia marefa kutoka nje ya nchi.
Ameitaka Bodi ya Ligi na mamlaka husika kuweka mkazo kwenye maadili (ethics), nidhamu na weledi katika upangaji na usimamizi wa marefa ili kuhakikisha michezo inaendeshwa kwa haki na viwango vinavyokubalika kimataifa.
Aidha, amesisitiza kuwa Wizara ina jukumu la kusimamia na kukuza sekta, huku akitarajia taasisi zinazosimamia soka kuchukua hatua madhubuti dhidi ya mapungufu yaliyopo, ikiwemo matumizi sahihi ya teknolojia kama VAR ili kuongeza uwazi na uaminifu katika maamuzi ya uwanjani.
WANAHABARI HAMISHENI AJENDA KWENDA KWENYE FURSA ZA KIUCHUMI.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, amewataka wanahabari kubadili mwelekeo wa maudhui kutoka kwenye “ku-brand watu” na siasa za kila siku, kwenda kwenye kuibua na kuonyesha fursa za kiuchumi zilizopo nchini.
Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani jijini Arusha, amesema Tanzania ina utajiri mkubwa wa vivutio vya utalii vinavyoweza kuwa chanzo kikuu cha mapato kwa vyombo vya habari iwapo vitapewa uzito wa kuripotiwa.
Ameeleza kuwa kwa sasa kuna upendeleo mkubwa wa kuripoti siasa kuliko sekta zenye tija kama utalii, jambo linalopunguza mchango wa vyombo vya habari katika kukuza uchumi wa Taifa na hata ustawi wa wanahabari wenyewe.
Aidha, amekemea tabia ya baadhi ya wanahabari kutumika kulinda maslahi ya watu binafsi, akisisitiza kuwa mwelekeo huo unadhoofisha taaluma na kuathiri uaminifu wa umma kwa vyombo vya habari.



Comments
Post a Comment