đź’˘ASISITIZA UADILIFU NA UHURU WA WAKAGUZI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI.
đź’˘TAKUKURU YAKAGUA MIRADI 164 YENYETHQMANI YA SHILINGI BILIONI 469. HUKU MIRADI 109 IMEKUTWA NA DOSARI.
Na Lucas Myovela - Arusha.
Mkuu wa Moa wa Arusha COA, Amos Makala, amesisitiza umuhimu wa viongozi na wadau kushirikiana kwa karibu katika utekelezaji wa majukumu yao, akieleza kuwa ushirikiano huo ni muhimu katika kukabiliana na vitendo vya rushwa kwenye miradi ya maendeleo na kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
CPA Makala ameyasema hayo mapema leo Agosti 10, 2026 wakati wa Warsha ya wadau wa usimamizi na utekelezaji wa Programu na Miradi ya Maendeleo Mkoa wa Arusha, warsha ambayo imewakutanisha viongozi na wadau mbalimbali wenye dhamana ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ambao baada ya kupata elimu na kujadili changamoto zilizopo, wanatarajiwa kwenda kutekeleza kwa vitendo.
Amesema viongozi ndio wenye dhamana ya kusimamia na kutekeleza miradi hiyo katika maeneo yao, hivyo wanapaswa kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa ufanisi, uwazi na kwa kuzingatia malengo yaliyokusudiwa.
“Ni lazima tuzungumze na tushirikiane, hasa katika masuala ya kupambana na rushwa kwenye miradi, lakini pia kuimarisha utoaji bora wa huduma kwa wananchi,” amesema.
Aidha CPQ, Makalla Amesisitiza Uadilifu na Uhuru wa Wakaguzi katika Usimamizi wa Miradi na amewataka watendaji wa Serikali kuzingatia uadilifu na kutekeleza majukumu yao kwa kufuata sheria, akisisitiza kuwa matumizi mabaya ya madaraka yanaweza kumuweka mtendaji katika hatari ya kuchukuliwa hatua za kisheria.
"Mtendaji anapaswa kuwa na hofu ya Mungu na kuzingatia sheria katika utekelezaji wa majukumu yake, huku akisisitiza umuhimu wa kutopindisha haki wakati wa kufanya kazi, wakaguzi wa Serikali kuweni makini na zawadi au huduma wanazopewa na pindi mnapo kwenda kuwafanya ukaguzi, kwenda kinyume na taratabu kwa kuwa kufanya hivyo kunaweza kuathiri uhuru na uadilifu wao katika kutekeleza majukumu". Amesema.
Amesema wakaguzi wanapaswa kulinda uhuru wao wa kitaaluma kwa kuepuka mazingira yanayoweza kuwafanya waonekane kuwa na maslahi binafsi katika taasisi au miradi wanayoikagua.
Akizungumzia usimamizi wa fedha za Serikali, amesema fedha nyingi zinatengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, hivyo ni muhimu taasisi zote zinazohusika kuhakikisha fedha hizo zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na wananchi wanapata thamani ya fedha.
Aidha meipongeza TAKUKURU kwa kuwakutanisha watendaji wa Serikali na taasisi mbalimbali katika warsha hiyo, akisema hatua hiyo imewapa fursa ya kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na namna ya kuzitatua.
“Tumekutana hapa, nimefurahi kuona wako kwenye mkutano huu viongozi wanaosimamia maeneo yao. Pia kuna taasisi mbalimbali. Tumekutana pamoja tukumbushane majukumu na uadilifu wa pamoja,” amesema.
"Fedha za Serikali ni za wananchi, hivyo kila mtendaji na taasisi yenye dhamana ya kusimamia fedha na miradi ya maendeleo inapaswa kuhakikisha inatekeleza majukumu yake kwa uadilifu, uwazi na kwa kuzingatia sheria". Ameongeza CPA Makala
Aidha, amewataka watendaji kuondoa mitazamo hasi kuhusu TAKUKURU, akisema taasisi hiyo haipaswi kuonekana kama chombo cha kuwazuia watendaji kutekeleza miradi, bali inapaswa kutazamwa kama mshirika katika kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa kuzingatia sheria na taratibu.
Amesema TAKUKURU inapaswa kuendelea kufuatilia miradi ya maendeleo na kutoa ushauri pale inapobaini changamoto, ili kasoro zinazoweza kuleta hasara au doa katika utekelezaji wa miradi ziweze kurekebishwa mapema.
“Takukuru wakiiona sehemu ambayo siyo nzuri, washauri. Lengo siyo kuzuia miradi, bali kuhakikisha miradi inatekelezwa vizuri na kwa kuzingatia taratibu,” amesema.
Ameongeza kuwa ushirikiano kati ya Serikali na TAKUKURU ni muhimu katika kuhakikisha miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa kwa kutumia fedha nyingi za umma inakuwa na tija kwa wananchi.
"Kwa msingi huo, amewataka washiriki wa warsha hiyo kutumia fursa hiyo kujenga mtazamo wa pamoja, kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi na kuhakikisha changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa miradi zinatatuliwa kwa wakati". Amesisitiza CPA Makala.
Kwa upande wake Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Arusha Zawadi Ngailo ameeleza kuwa tasisi hiyo uwa inatumia mbinu mbbalimbali za ufatiliaji wa matumizi ya Rasilimali za umma katika utekelezaji na usimamizi wa programu na miradi mbalimbali na kisha kuzishauri taasisi husika juu ya mapungufu,changamoto ambazo wanazibaini katika miradi husika.
"Katika kipindi cha mwaka wa frdha 2023/2024, 2024/2025 na 2025/2026, Ofisi imefuatilia matumizi ya rasilimali za umma katika program miradi na miradi ya maendeleo 164 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 469.9. Miradi 109 ilikutwa na dosari ambazo zilitolewa mapendekezo 452 ya kuboresha miradi". Amesema Ngailo.
Ngailo ameeleza kuwa kutokana na changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikibainika katika baadhi ya miradi ya maendeleo inayofuatiliwa, hali ambayo imekuwa changamoto kubwa katika usimamizi na utekelezaji wa programu za miradi hiyo ikiwemo ucheleweshaji wa upatikanaji wa rasilimali fedha, uchanganyaji wa baadhi ya miradi pamoja na ushiriki mdogo wa wadau katika usimamizi na ufuatiliaji zimekuwa zikisababisha baadhi ya miradi kutekelezwa nje ya muda uliopangwa au kukumbwa na vikwazo mbalimbali.
Amesema miongoni mwa matarajio ya warsha hiyo ni kuhakikisha programu na miradi ya maendeleo inatekelezwa bila ucheleweshaji wa upatikanaji wa rasilimali fedha, kupunguza ucheleweshaji wa miradi pamoja na kuongeza ushiriki wa wadau katika kusimamia na kufuatilia utekelezaji wake.
Aidha Ngailo ameeleza kuwa mikakati hiyo inatarajiwa kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi na kuhakikisha kila mdau anashiriki kikamilifu katika usimamizi wa miradi, ili kuwepo kwa thamani ya fedha iliyotengwa na kutumika katika utekelezaji wa miradi husika.
Ameeleza kuwa wadau wenye dhamana ya usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo wanapaswa kutekeleza majukumu yao kwa pamoja, kuhakikisha miradi inasimamiwa kwa kuzingatia thamani na malengo yaliyokusudiwa, na hatimaye wananchi wanapata maendeleo yanayolengwa.
Pia Ngailo amewataka wadau kuendelea kushirikiana kwa karibu na kwa wakati wote katika kutekeleza jukumu la kuzuia vitendo vya rushwa, akisisitiza kuwa mapambano dhidi ya rushwa ni wajibu wa kila mmoja.
Comments
Post a Comment